December 10, 2015

HILI NDILO BARAZA LA MAWAZIRI LA TANZANIA LILILOTANGAZWA NA RAIS DKT. MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Leo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli ametangaza Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kabla ya kulitangaza ameeleza yafuatayo;-
 
"Watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.  

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.  

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani"

WIZARA NA BARAZA LA MAWAZIRI

Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora: Mawaziri ni George Boniface Taguluvala Simbachawene na Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Naibu waziri Selemani Saidi Jafo.  

Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Waziri ni January Yusuf Makamba, naibu Luhaga Mpina 

Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Jenista Joakim Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Abdallah Possi. M ambae ni mhadhiri Dodoma  

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Waziri ni Jenista Muhagama, manaibu Anthony Mavunde, Possy Abdallah.  

Kilimo, mifugo na uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, naibu William Ole Nasha 

Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri mhandisi Edwin Ngonyani. 

Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Ashantu Kizachi  

Nishati na madini: Waziri ni Professa Sospeter M. Muhongo, Naibu waziri ni Medadi Kalemani  

Katiba na sheria: Waziri Harrison George Mwakyembe  

Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa: Waziri ni Augustine Philip Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.  

Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Ali Mwinyi  

Mambo ya ndani: Charles Muhangwa Kitwanga  

Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi: Waziri ni William Vangimembe Lukuvi, Naibu Angelina Mabula  

Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala  

Viwanda, biashara na uwekezaji: Waziri Charles John Poul Mwijage  

Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya 

Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto: Waziri Ummy Ally Mwalimu, Naibu ni Hamisi Andrea Kigwangalla  

Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Waziri Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura 

Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mnyaa Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Isack Kamwela