November 24, 2015

WAKENYA WAMTAMANI DKT. MAGUFULI AWE RAIS WAOKwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Rais Dk. John Magufuli amefanya mambo kadhaa ambayo yamekuwa gumzo nchini. Kutokana na mambo hayo yaliyoorodheshwa hapo chini, Wakenya wamemkubali Magufuli na kuelezea hisia zao za kumtamani angekuwa rais wa nchi yao. Mambo hayo ni:-

1. Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili  ilivumbua vitu vingi na kumpelekea Rais Magufuli kufuta bodi ya Wakurugenzi wa hospitali hiyo pamoja na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk. Hussein Kidanto. 

2. Kufuta safari za viongozi kwenda nchi za nje ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa za Serikali. 

3. Alielekeza shilingi milion 225 zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla ya Pongezi za Wabunge Dodoma kutumika kununua vitanda vya hospitali na shilingi milion 15 tu ndio zitumike kwaajili ya sherehe hiyo. 

4. Jumatatu ya tarehe 23 November 2015, Rais Dk. John Magufuli alitangaza kufuta kwa sikukuu ya Uhuru December 9 na kuagiza fedha za maandalizi ya sikukuu hiyo zitumike kutatua matatizo mengine pia ameagiza siku hiyo itumike kusafisha mazingira ili kupunguza matatizo ya kipindupindu nchini.

TWEETS ZA WAKENYA HIZI HAPA