November 17, 2015

TAARIFA KUTOKA TANESCO


TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA NOVEMBA 22, 2015 ILI KURUHUSU MKANDARASI KUUNGA LINE KUBWA YA BACKBONE KWENYE KITUO CHA KUPOOZEA NA KUSAMBAZA UMEME CHA IRINGA MJINI. 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa mikoa ya Iringa, Mbeya, Dodoma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Manyara, Simiyu na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kuwa yatakosa umeme siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni ili kuruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo wa Kilovolti 220 maarufu kama Backbone kutoka Iringa kwenda Shinyanga, kuunga njia hiyo kwenye Kituo cha Kupoozea na Kusambaza Umeme cha Singida.

Mradi huo wa Backbone unalenga kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini na utekelezaji wake upo katika hatua nzuri.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na:

Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO - MAKAO MAKUU.