November 23, 2015

KILIMANJARO STARS YAISHUSHIA KICHAPO CHA MBWA MWIZI SOMALIA- CECAFA

Michuano ya mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA iliendelea kwa michezo miwili kupigwa, timu ya taifa ya Tanzania bara inayofahamika kama Kilimanjaro Stars ilishuka dimbani kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Somalia .

Kilimanjaro Stars ambayo ndio imecheza mchezo wake wa kwanza November 22 imeibuka na ushindi mnono wa magoli manne 4-0 dhidi ya Somalia ambapo magoli hayo yakifungwa na Bocco magoli mawili na Maguli magoli mawili.