November 16, 2015

JOB NDUGAI APITISHWA NA CCM USPIKA WA BUNGE LA JMT

Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya jina lake kupitishwa kama mgombea wa Uspika.

Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.

“Kama tulivyoona wagombea wawili walijitoa, hivyo Job Ndugai amepitishwa kwa kauli moja kugombea nafasi ya uspika. Tunamuombea kura kwa sababu sifa zote anazo, bila shaka hakutatokea mgombea wa upinzani atakayezidi sifa zake,” alisema Nape.