November 19, 2015

HUYU NDIYE ALIYETEULIWA NA MHE RAIS KUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA

Kassim Majaliwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemteua ndugu Kassim Majaliwa kuwa ndiye Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika bahasha iliyotumwa kwa Spika wa bunge ndani kulikuwa na barua iliyoandikwa kwa mkono wake mwenyewe Rais na si kwa kuchapwa ambayo ilisomeka kama ifuatavyo...

'' Job Ndugai, Mh Spika, mimi mwenyewe kwa nafasi yangu kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimemteua Mbunge wa Ruangwa mh. Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.''