October 13, 2015

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAWAONDOA WATU MILIONI MOJA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

Tume inayosimamia uchaguzi nchini Tanzania (NEC), imefuta majina ya wapiga kura zaidi ya milioni moja kutoka kwenye orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura.

Awali tume hiyo ilikuwa imetoa idadi ya wapiga kura milioni 23.7 waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu kupitia kwa mfumo wa kielektroniki (BVR).

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema idadi hiyo imepigwa kalamu kufuatia shughuli ya kuhakiki majina ya watu wote waliojiandikisha.

Majina ya watu milioni moja, 1,031,769 waliopatikana kuwa na makosa moja au zaidi yaliondolewa.

Chanzo: BBC Swahili