October 1, 2015

LUBUVA AWAONDOA HOFU WAPIGA KURA


KALAMU YOYOTE ITATUMIKA KUPIGIA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU 2015

Ili kuondoa shaka miongoni mwa wananchi kutokana na tetesi zinazosambazwa juu ya ubora wa kalamu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kila mtu anaruhusiwa kuja na kalamu yake kupigia kura Oktoba 25, mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na NEC wakati ilipofanya mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari nchini ikiwa ni siku ya tatu ya kukamilisha utaratibu wa kuzungumza na wadau wa uchaguzi baada ya kufanya hivyo kwa wawakilishi wa walemavu na wamiliki wa vyombo vya habari nchini.

Akisisitiza juu ya ushiriki wa wadau kutoa elimu ya mpiga kura, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lubuva amesema kipindi hiki cha kampeni kimeshuhudia kuzuka kwa maneno mengi yasiyokuwa na uhakika ambayo yanawachanganya wananchi.