October 13, 2015

BALAA: KIGOGO MWINGINE AJITOA CCM

Balozi Juma Mwapachu

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Juma Mwapachu leo ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kutokana na chama kupoteza dira.

Tamko la Balozi Mwapachu linasema kuwa kuanzia kesho kada huyo wa CCM hatakuwa tena mwanachama wa chama hicho tawala na kuongeza kuwa bado hajaamua kujiunga na chama kingine.

‘’Kuanzia kesho mimi si mwana CCM tena. Nitarejesha rasmi kadi yangu kupitia ofisi ya CCM ya kata yangu Mikocheni, Dar es Salaam. Kwa sasa sijaamua kujiunga na chama kingine. Mwenyezi Mungu anilinde,” inasema sehemu ya tamko hilo.

Chanzo: Mwananchi