September 24, 2015

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI& TATU 2015 NA WALIOBADILISHIWA SHULE


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU – TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WANAFUNZI WALIOBADILISHIWA SHULE, TAHASUSI NA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI 2015

Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imefanya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili 2015 ambapo wanafunzi 4775 (Wavulana 3,211 na Wasichana 1,564) wamechaguliwa . Aidha, wanafunzi wote 305 walioomba kubadilisha shule na tahasusi (sanaa kwenda sayansi) wamebadilishiwa. Uchaguzi na mabadiliko hayo umezingatia nafasi zilizopatikana baada ya baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa awamu ya kwanza kushindwa kuripoti. Wanafunzi hao wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe 14/09/2015 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 28/09/2015.

Kwa tangazo hili Wakuu wa shule mnatakiwa kuwaruhusu kuondoka/ kuwapokea wanafunzi waliopangwa au kubadilishiwa shule/tahasusi bila pingamizi lolote. Wazazi/Walezi mnashauriwa kuwasaidia wanafunzi ambao wamebadilishiwa shule. Aidha, wanafunzi ambao wameridhika na tahasusi wanazosoma kabla ya tangazo hili wasilazimishwe kuondoka.

Imetolewa na Katibu Mkuu
OFISI YA WAZIRI MKUU – TAMISEMI
11 SEPTEMBA, 2015

KUFUNGUA MAJINA BOFYA KWENYE LINKI HIZO HAPO CHINI

  1. ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI SEPTEMBA 2015 
  2. ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO AWAMU YA TATU SEPTEMBA 2015