September 10, 2015

TANGAZO LA KUITWA MAFUNZONI IDARA YA UHAMIAJI

 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
IDARA YA UHAMIAJI
KUITWA MAFUNZONI

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia wote waliofaulu usaili wa nafasi za ajira ya Konstebo, Koplo na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji ulioendeshwa katika Kambi na Vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwa wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Mtaa wa Loliondo Kurasini Dar es salaam Siku ya Alhamisi, Tarehe 10 Septemba, 2015 kwa ajili ya maandalizi ya safari ya kwenda kujiunga na Shule ya Polisi- Moshi hapo Tarehe 11 Septemba, 2015.

Mahitaji na vifaa muhimu wanavyopaswa kuandaa na kuwa navyo huko Shule ya Polisi Moshi ni pamoja na:
  • Mashuka mawili (2) rangi ya blue bahari (light blue);
  • Chandarua chenye upana wa futi 3;
  • Nguo za michezo (track suit nyeusi, T-shirt ya rangi ya blue na raba za michezo);
  • Pasi ya mkaa;
  • Ndoo moja;na
  • Pesa ya tahadhari Shilingi 50,000/= na
  • Nauli ya kuwawezesha kufika Shule ya Polisi Moshi.
Atakayesoma tangazo hili amjulishe na mwingine.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI
LEO TAREHE 08 SEPTEMBA, 2015