September 2, 2015

TAARIFA YA CHADEMA/UKAWA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kutokana na vyombo vya habari mbalimbali kutaka kauli yetu kuhusu mkutano wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Willbroad Slaa na waandishi wa habari uliofanyika jana Hoteli ya Serena na kutangazwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na radio, tunapenda kusema ifuatavyo;

Tumemsikia Dkt. Slaa. Kwa sasa nguvu, akili, mioyo na miili ya wapiganaji wa CHADEMA imeelekezwa kwenye kampeni, kushinda uchaguzi huu kwa ajili ya kuleta mabadiliko ambayo Watanzania wanayahitaji sana, wanayaunga mkono na wako tayari kuyapigia kura hapo Oktoba 25, kwa sababu wakati wake ni huu.

Wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA wakishirikiana na wenzao wa vyama vinavyounda UKAWA, wanaendelea kujikita katika mikakati ya kutafuta ushindi wa Mgombea Urais, Edward Lowassa akiwa na Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji halikadhalika wabunge na madiwani nchi nzima.

Imetolewa leo Jumatano, Agosti 2, 2015 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano