September 6, 2015

TAARIFA HII YA NEC INALETA MATUMAINI KWA WAPIGA KURA OKTOBA 25
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania (NEC) imewahakikishia Watanzania wote waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR kuwa watapiga kura.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bi. Giveness Aswile ametoa hakikisho hilo wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya zoezi la uhakiki wapiga kura linaloendelea nchini nzima na kuongeza kuwa hata wale ambao taarifa zao zilikosewa kwa bahati mbaya wakati wa kuandikishwa watapiga kura na kuongeza kuwa kukosewa kwa taarifa zao hakutawanyima sifa na haki yao ya msingi ya kupiga kura. 

Bi. Giveness amesisitiza kuwa pindi daftari la wapiga kura litakapo kamilika vyama vyote vya siasa nchini vitapewa ili walitumie wakati wa kupiga kura ili kuondoa wasiwasi wa kuwepo kwa wapiga kura wasio na sifa katia daftari hilo.