September 12, 2015

MWAKALEBELA AFUNIKA IRINGA

MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Iringa kupitia chama cha mapinduzi ( CCM) Frederick Mwakalebela amesema jimbo la Iringa Mjini limekosa kunufaika na fursa za maendeleo kwa kuwa halikuwa na mbunge makini wa kuleta maendeleo.  Hivyo amewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuacha kujutia kukosa maendeleo na badala yake kumchagua yeye kuwa mbunge wao ifikapo Octoba 25 mwaka huu.

Mwakalebela ametoa kauli hiyo leo wakati wa mkutano wake wa kampeni za Ubunge kwenye kata ya Mshindo alisema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anasogeza maendeleo ya haraka kwa wananchi wa Jimbo la Iringa ambao kwa miaka mitano wamekosa kupata maendeleo hayo .