September 14, 2015

MANENO YA MBOWE KWENYE MSIBA WA MTOI YAMLIZA YEYE NA WAOMBOLEZAJI: SOMA HAPA ALICHOKIONGEA

Maneno ya Mbowe

"Nimesafiri na Mtoi mikoa yote Tanzania, nilimpebda kwa uadilifu wake, kwa mara ya mwisho nilionana naye ijumaaa 06:25 Jioni pale Makao Makuu, alikuja akakuta mimi nina Kikao, Mtoi akalazimisha walinzi kuwa ni lazima anione.. Wakamkatalia coz nilikuwa na meeting, mtoi hakukubali akasema lazima nionane na mwenyekiti, wakamruhusu, akaingia ndani, nikasimamisha kikao Mtoi ili aongee, akasema samahani mwenyekiti Sina issue kubwa ila nimekuja kukuaga naenda lushoto, naenda kuzindua kampeni, nikamuangalia nikasema huyu dogo Atakuwa na shida fulani anazuga tu, nikamuuliza mtoi Sema una shida gani? Una shida na pesa kiasi gani na kwanini uende Lushoto usiku huu ? Akajibu mwenyekiti Sina shida yoyote.. Nasema hivi nimekuja kukuaga ni lazima niende usiku huu coz kesho nazindua kampeni, kumbe kweli mtoi ndo alikuwa ananiaga kwa style hiyo. Amezindua kampeni jmosi na kufariki siku hiyo hiyo."

Baada ya maneno hayo ya Mbowe watu wakaanza kulia Tena.