September 17, 2015

MAGUFULI AFANYA YAKE KIGOMA

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kigoma ambapo aliwaambia atajenga Tanzania mpya yenye uchumi wa Viwanda.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Alhaji Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Kawawa, Ujiji mkoani hapo.
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Yusuph Makamba akihutubia wakazi wa Kigoma ambapo aliwaambia wasidanganyike na wanasiasa wasiojua historia ya jambo.
 Msanii Joti akionyesha uwezo wake kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli uliofanyika viwanja vya Kawawa, Ujiji mkoani Kigoma.
 Wasanii wa Ze Komedi wakionyesha uwezo wao wa kucheza kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli.