September 26, 2015

HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA BARCELONA JUU YA LIONEL MESSI

Mchezaji Leonel Messi wa Barcelona amelazimika kutolewa nje ya uwanja dakika ya kumi baada ya kupata maumivu ya mguu wakati wa mchezo kati ya Barcelona dhidi ya Las Palmas mchezo wa ligi kuu Hispania.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba Lionel Messi atakuwepo nje ya uwanja kwa muda wa wiki Saba au nane(Miezi miwili) jambo ambalo litaleta hofu kwa mashabiki wa Barcelona kwani Messi amekuwa ni mchezaji mwenye mchango mkubwa katika timu.