August 28, 2015

ZITTO KABWE ATUMIA MBINU HII KUSHINDA MAJIMBO MENGI ACT

Kiongozi mkuu wa ACT akitoa maelekezo kwa wagombea wa ACT kuelekea uchaguzi mkuu.

Chama cha ACT wazelendo leo kimenza mafunzo ya siku mbili mfululizo kwa wagombea wake wa nafasi za ubunge nchini mafunzo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo na kujiamini zaidi kuelekea kufanya kampeni na kutafuta nafasi za uwakilishi wa katika majimbo mbalimbali kikiwa ni chama pekee nchini Tanzania kulichoendesha mafunzo kama hayo kwa sasa.

Kiongozi mkuu wa chama hicho ZITTO ZUBER KABWE akizungumza na wanahabari wakati wa mafunzo hayo amesema kuwa chama hicho ni chama pekee nchini Tanzania kilichodiriki kuwapa mafunzo ya kuelekea katika uchaguzi ili kuwaweka katika mstaari mmoja wa kuhakikisha kuwa wanakwenda na lugha moja kwa watanzania kueleza mipango na ilani ya chama hicho.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo na kujiamini zaidi kuelekea kufanya kampeni na kutafuta nafasi za uwakilishi wa katika majimbo mbalimbali kikiwa ni chama pekee nchini Tanzania kulichoendesha mafunzo kama hayo kwa sasa.