August 28, 2015

MESSI ANYAKUA TUZO NA KUMBWAGA RONALDOMshambuliaji wa Barcelona na Nahodha wa Argentina, Lionel Messi amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka 2014/2015 barani Ulaya. Messi amewashinda Christiano Ronaldo na Luis Suarez katika kinyang'anyilo hicho.

Messi ameshaanza msimu huu kwa kupachika mabao mawili dhidi ya Sevilla huku mpinzani wake Ronaldo akionekana kuzidi kuwa butu na kukabika kirahisi tofauti na miaka ya nyuma.