August 26, 2015

MASHA ADHAMINIWA

Masha aliyevaa tisheti jeusi suruali ya jinsi ya rangi ya Bluu akifurahia jambo na wenzake


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha (45) baada ya kukamilisha masharti ya dhamana. Masha alifikishwa mahakamani hapo jana nyakati za saa 6:49 mchana na kuhifadhiwa mahabusu na ilipofika saa 9:31 alasiri alipelekwa mbele ya Hakimu Mkazi  Mkuu, Waliarwande Lema kwa ajili ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Masha alikuwa huru baada ya nyaraka za wadhamini wake wawili wanaoaminika ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh 1milioni kuhakikiwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon
kuithibitishia mahakama kuwa nyaka hizo ni halali. Kufanyika kwa uthibisho huo wa nyaraka za wadhamini ndio uliopelekea juzi Masha kupelekwa mahabusu katika gereza la
Segerea.

Baada ya kumaliza kukamilisha taratibu hizo za dhamana ilipofika saa 9:46 alasiri Masha, mkewe, mawakili wanaomtetea katika kesi hiyo, Peter kibatala na Albart Msando pamoja na ndugu zao wengine waliondoka mahakamani hapo kwenda nyumbani.

Chanzo: Mwanchi