August 22, 2015

FREDRICK MWAKALEBELA AOMBA RADHI KWA ALICHOKIWEKA FACEBOOK


Hiki ndicho alichokiandika facebook


"Za asubuhi ndugu zangu! Awali ya yote naomba niombe radhi kwa kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na post iliyopita,Binafsi naomba kukanusha iyo post imewekwa pasipo idhini yangu,account hii ya FB ni yangu ila kilichotokea kuna mtu amepost kwa niaba yangu huo ujinga uliopitiliza,baada ya kuwa busy na michakato ya Siasa niliona ni jambo la busara kuwatafuta vijana wa kuendesha kurasa zangu za mitandao ya kijamii lakini kumbe nao wamenigeuka na kuanza kunichafulia jina langu,Kwa mara nyingine tena naomba kutumia nafasi hii kuwaomba radhi wale wote walioathirika kwa namna moja ama nyingine."