July 20, 2015

SILAHA ZILIZOIBWA NA MAJAMBAZI WALIOUA STAKISHARI ZAKAMATWA


Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam akiwaonyesha wanahabari silaha bunduki 16 zilizokutwa zimefukiwa chini huko pwani mkuranga huku bunduki 14 zikiwa ni zile zilizoporwa katika shambulio la kuvamiwa kituo cha polisi stakishari jijini Dar es salaam
Hili ndio sanduku lililokua limehifadhi pesa taslimu million 170 na kufukiwa chini huko mkurangaDar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata bunduki 14 na risasi 28 zilizoporwa katika kituo cha polisi cha Stakshari. Sambamba na silaha hizo ambazo ni bunduki za SMG 7, bunduki za SAR 7 zote zikiwa zimeibiwa Stakshari, jeshi hilo pia limekamata bunduki ya kichina aina ya Norinko  na  sanduku la chuma lililosheheni fedha za kitanzania 170 milioni.

Kamishina wa Polisi, ACP Suleiman Kova amesema leo pamoja na kukamata sialaha hizo, jeshi hilo linawashikilia watu wawili kati ya watano waliokamatwa wakijiandaa kufanya uhalifu eneo la Toangoma jijini Dar es Salaam. Kova alisema watu watatu kati yao walifariki dunia baada ya kupambana na Polisi waliokuwa wakitaka kuwaweka nguvuni baada ya kubaini mpango wao wa kufanya uhalifu.