May 24, 2015

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU AWAMU YA PILI (NACTE).ORODHA YA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJINGA NA MAFUNZO YA UALIMU AWAMU YA PILI MWAKA WA MASOMO 2014/2015

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi limechagua waombaji 2,543 (Me 1,651 na Ke 892) kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Awamu ya Pili ya Mwaka wa Masomo 2014/2015. Waombaji 1,968 (Me 1226, Ke 742) wamechaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa wanachuo (Central Admission System – CAS) na waombaji 575 (Me 425,Ke 150) wamechaguliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Waombaji wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ualimu vya Butimba, Tabora, Tukuyu, Mpwapwa, Kinampanda, Mhonda, Nachingwea, Singachini na Tandala. Vyuo vingine ni Tarime, Bustani, Marangu, Morogoro, Klerru na Songea. Mafunzo ya Ualimu yataanza tarehe 01/06/2015, hivyo wanachuo wanatakiwa kuanza kuripoti vyuoni kuanzia tarehe
28/05/2015. Fomu za Maelekezo ya Mafunzo (Joining Instructions) yameambatishwa. Pamoja na maelekezo yaliyopo kwenye fomu za kila chuo, mwanachuo anatakiwa kuripoti chuoni akiwa na vyeti halisi vya masomo na kwa ajili ya taratibu za usajili.

Mwombaji yeyote aliyechaguliwa ambaye chuo chake si miongoni mwa vyuo vilivyotajwa ataweza kuomba uhamisho kwenye vyuo tajwa kwa kuandika barua au kupiga simu 0768 614045 la sivyo atajiunga na masomo mwezi Septemba 2015. Mwisho wa kupokea maombi ya uhamisho ni tarehe 25 Mei 2015.


IMETOLEWA NA:
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE 15/05/2015

Kufungua Orodha Ya Waliochaguliwa Kujiunga Na Masomo Ya Ualimu (NACTE). BOFYA HAPA