May 25, 2015

TANGAZO KWA KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA NA VITUO WALIVYOPANGWA


MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA ANA WATANGAZIA VIJANA IDADI 20000 WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA MEI 2015 KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA. WANATAKIWA KURIPOTI KWENYE VIKOSI VYA MAFUNZO WALIVYOPANGIWA KUANZIA TAREHE 08 JUNI 2015. MAFUNZO YATAANZA RASMI TAREHE 15 JUNI 2015 NA KUMALIZIKA TAREHE 15 SEPTEMBA 2015.
YAFUATAYO YAZINGATIWE
  1. VIJANA WANAOTAKIWA KUJIUNGA WAWE RAIA WA TANZANIA
  2. WARIPOTI WAKIWA NA VYETI HALISI VYA KUZALIWA NA KUMALIZA KIDATO CHA SITA (LEAVING CERTIFICATE).
  3. VIJANA WENYE ULEMAVU UNAOONEKANA WARIPOTI KWENYE KIKOSI CHA RUVU.
  4. WALE WENYE MATATIZO AMBAYO YATAPELEKEA KUTOKUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KWA SASA WAANDIKE BARUA YA MAOMBI YA KUAHIRISHA MAFUNZO KWA MKUU WA JKT WAKIAMBATISHA VIELELEZO VYA TATIZO ALILONALO. MWAWASILIANO YOTE YAFANYIKE KUTUMIA ANUANI IFUATAYO.

MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA
MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA
S.L.P 1694
DAR ES SALAAM.


TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA