May 21, 2015

MICHEZO: DAVID LUIZ AELEZA KUWA HATOFANYA MAPENZI HADI AFUNGE NDOAMchezaji wa zamani wa Chelsea beki David Luiz amebaini mipango yake ya kuacha ngono mpaka yeye kuoa mpenzi wake Sara Madeira .

Luiz mwenye umri wa miaka 28 alitoa tangazo sambamba na picha yake aliyoipost Instagram akijionyesha tukio la kubatizwa katika bwawa la kuogelea la mchezaji mwenzake Maxwell.

Yeye mara nyingi husema juu ya imani yake ya Kikristo, na kutangaza kuwa yeye amechagua kusubiri hadi afunge ndoa na mpenzi wake wa kireno Sara Madeira.

Katika post yake Instagram, sambamba na tamko lake katika kuthibitisha yeye amechagua kusubiri , alitoa mfano wa aya kutoka Wakorintho : “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita Tazama! yamekuwa mapya . "