May 24, 2015

KIONGOZI WA UPINZANI BURUNDI ZEDI FERUZI APIGWA RISASI NA KUFAZedi Feruzi , kiongozi wa chama cha upinzani, amepigwa risasi na kufa sambamba mlinzi wake mjini Bujumbura, uongozi wa juu wa upinzani umethibitisha kwa Al Jazeera.

Feruzi , ambaye mwili wake ulikutwa umetapakaa damu alipatikana katika wilaya Ngagara ya Bujumbura siku ya Jumamosi jioni , alikuwa mkuu wa Chama cha Upinzani cha Union Peace and Development ( UPD ). 

Kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa , alisema hakuna taarifa juu ya ambaye amehusika kumuuawa Feruzi , lakini yeye alikuwa amesema na kupinga dhidi ya uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza ya kusimama kwa mara ya tatu katika kugombea urais.

Wakazi alisema mtu wa tatu , inaaminika kuwa afisa wa polisi mwingine ambaye inaaminika alikuwa na nia ya kumuokoa na kumlinda Feruzi alijeruhiwa vibaya katika tukio hilo.

"Tulisikia karibu  milio 20 ya risasi , kila mtu akaanguka chini , watu wakaona gari aina ya Toyota likiwa kasi linaondoka ," walisema majirani , ambao hawakuwa na ushahidi juu ya warushaji wa risasi

Karibu saa baada ya shambulio hilo polisi walikuwa bado kufika katika eneo la tukio , kwa mujibu wa shirika la habari AFP . 

Mauaji ya Jumamosi yataongeza mvutano nchini Burundi baada ya mwezi wa maandamano dhidi ya Rais Nkurunziza .  

Jaribio la mapinduzi ya kumuondoa Nkurunziza na maafisa wa jeshi kinyume na uamuzi wake wa kugombea urais yalishindwa baada ya kuingilia kati kwa wanachama waaminifu wa kijeshi. 

Zaidi ya watu 20 wamefariki dunia katika maandamano dhidi ya serikali tangu kutangazwa rais kusimama tena kuwania urais awamu ya tatu mwishoni mwa mwezi Aprili.

 Chanzo: Al Jazeera And AFP