May 21, 2015

AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI - MEI 2015

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli anawatangazia wananchi wote wenye sifa zilizoanishwa hapa chini kutuma maombi ya kazi kame'! zilivyotangazwa:-
 
1.Afisa Mtendaji Kijiji Daraja III - Nafasi 10
Ngazi ya Mshahara TGS B 1

Sifa :
Mwombaji lazima awe amemaliza Elimu ya kidato cha nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. 
 
Umri: Mwombaji awe na umri kati ya miaka 18 - 40.
Waombaji wote wenye na sifa zilizoainishwa walioajiriwa, wapitishe barua zao kwa waajiri wao, waambatishe nakala za vyeti vya mafunzo, passport size 2 namba ya simu na CV.
 
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe05/06/2015 saa 9.30 alasiri.
APPLICATION INSTRUCTIONS:
Maombi vote yatumwe kwa;
 
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya Monduli,
S. L. P. 1,
MONDULI.

 
Limetolewa na: 
Dominic M. Msagati.
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI (W),
MONDULI