November 23, 2016

TANGAZO MUHIMU LA VIJANA KUJIUNGA NA JKT


TAARIFA KWA UMMA

1.    Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawatangazia vijana wa Kitanzania wito wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya pili na Vijana wa Kujitolea.

2.    Vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo ni kama ifuatavyo:-

      a.   Vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli Awamu ya Pili.
             Kundi hili linahusisha wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016, ambao hawakuchaguliwa kwenye mafunzo ya JKT Mujibu  wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya kwanza na hawakupata nafasi ya kujiunga vyuo vya elimu ya juu. Aidha, orodha kamili ya majina na makambi waliyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Jeshi la Kujenga Taifa, ambayo ni www.jkt.go.tz  na Tovuti Kuu ya Serikali www.tanzania.go.tz

      b.      Vijana wa Kujitolea
Kundi hili linahusisha Vijana wote waliosailiwa mwezi Mei na  Juni mwaka 2016 katika ngazi za wilaya na mkoa  na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.
3.   Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na Kujitolea wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa wakiwa na vifaa vifuatavyo:
      a.  Bukta ya rangi ya bluu iliyokoza (Dark blue) yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma isiyo na zipu, iwe na urefu  unaoishia magotini.                 

       b.  Raba ngumu za michezo zenye rangi ya kijani au nyeusi.

       c.  Shuka jozi mbili za kulalia zenye rangi ya bluu bahari ukubwa wa 4x6.
       d.  Soksi za michezo jozi mbili rangi nyeusi.

       e.  Chandarua moja ya duara rangi ya bluu au kijani ukubwa wa 4x6.

        f.  Nguo za michezo (truck suit) jozi moja rangi ya kijani au bluu.

        g.  Fulana (T-shirt) ya kijani isiyokuwa na maandishi yoyote.

        h.  Mavazi hayo yasiwe ya kubana mwili.

4.  Inasisitizwa kuwa vijana wa kujitolea wanaotakiwa kuripoti makambini ni wale tu waliopita katika usaili kwenye ngazi
za wilaya na mikoa na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.

5.  Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na  Kujitolea wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia
tarehe 01 mpaka 05 Desemba 2016 kwa kujitegemea nauli ya kwenda na kurudi.

 BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI  KUANGALIA MAJINA JA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI  2016  

BULOMBORA JKT-KIGOMA                           RWAMKOMA JKT -MARA                  MSANGE JKT-TABORA

KANEMBWA JKT-KIGOMA                                         MTABILA-KIGOMA                      RUVU JKT-PWANI

MAKUTUPORA JKT- DODOMA                           MGAMBO JKT-TANGA              MARAMBA JKT- TANGA

MAFINGA JKT- IRINGA                                                                                MLALE JKT -RUVUMA


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 17 Novemba 2016

October 30, 2016

BREAKING NEWS: AJALI YA BASI, GARI LAUNGUA PAMOJA NA ABIRIA WAKIWA NDANI YA GARI

Ajali mbaya sana imetokea eneo la Suca mbele kidogo ya Stop Over ikihusisha lori na Basi T 990 ADF liitwalo Safari Njema linalofanya safari zake kati ya Dar na Dodoma ambapo basi hilo linaungua pamoja na watu waliomo ndani ya gari. Vichwa vya watu vinasikika vikipasuka kwa milipuko mikubwa.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba dereva wa basi alikuwa anaovertake eneo hilo la gereji ambalo barabara ni nyembamba sana na magari hupita kwa mwendo kasi mkubwa.

Picha zote hapa chini....Taarifa kamili zitakujia hapo baadaye.

October 26, 2016

MPIGIE KURA RAIS MAGUFULI ASHINDE FORBES AFRICA PERSON OF THE YEAR


Mpigie kura Rais wetu aweze kushinda kwenye Forbes Africa Person of the year. Siku ya mwisho kupiga kura ni tarehe 01 Novemba 2016
KUINGIA KWENYE TOVUTI YA KUPIGA KURA  BOFYA HAPA.

October 25, 2016

FORBES: RAIS MAGUFULI KUWANIA TUZO YA MTU MASHUHURI


Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania tuzo la Forbes la mtu mashuhuri wa mwaka. Jarida hilo la biashara limemtambua rais Magufuli kwa umuhimu wake katika kuimarisha uchumi wa taifa hilo.

Wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Benki ya Capitec nchini Afrika Kusini,rais wa Mauritania,Mtetezi wa haki za umma nchini Afrika Kusini na raia wa Rwanda. Mwaka uliopita tuzo hilo lilichukuliwa na mfanyibiashara wa Tanzania Mohammed Dewiji.